Posts

Showing posts from September, 2020

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.09.2020: Sancho, Jovic, Alaba, Tagliafico, Lamptey

Image
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Sancho alijiunga na Dortumund akitokea Manchester City mwezi Agosti mwaka 2017 Ofa ya Manchester United ya pauni milioni 91.3 kwa ajili ya mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20 imekataliwa na Borussia Dortmund. (Sky Sports) Na United inahofia kushusha thamani yake ikiwa ofa yake ngingine kwa ajili ya Sancho itakataliwa na Dortmund. (Mail) Pia wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Real Madrid na Serbia Luka Jovic, 22, kwa mkopo. (AS - in Spanish) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Luka Jovic Na inakaribia kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 23, - wakiipiga Barca jeki kifedha kumsajili mshambuliaji wa Lyon aliyekuwa Manchester United Memphis Depay. (AS - in Spanish) Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamewasiliana na Brighton juu ya uwezekano wa makubaliano na beki wa kulia Tariq Lamptey, 19. (Sport1, via Metro) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Ma...

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 29.09.2020: Sancho, James, Aarons, Skriniar, Zouma

Image
CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha, Jadon Sancho alijunga na Borussia Dortmund kutoka Manchester City msimu wa mwaka 2017 Manchester United haijakata tamaa katika mbio zao za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Uingereza Jadon Sancho, 20. (ESPN) Tottenham inafikiria kumchukua tena mlinzi wa Inter na Slovakia Milan Skriniar, 25, lakini haiko tayari kumsajili kwa bei yake. (Guardian) Barcelona inakaribia kufikia makubaliano ya mwisho na Ajax kuhusu beki wa kulia wa Marekani Sergino Dest, 19, lakini ina uwezo mdogo wa kufanya makubaliano zaidi ya usajili. (Goal) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Daniel James atajiunga na Leeds kwa mkopo Manchester United itamruhusu winga raia wa Wales Daniel James, kujiunga na Leeds United kwa mkopo, lakini kama watamsajili Sancho. (Sun) Everton na Leicester City zote zinamnyatia mlinzi wa Chelsea raia wa Ufaransa Kurt Zouma, 25. (Le10 Sport, via Talksport) Sheffield United imetoa ofa kwa Liverpool ya pauni milio...

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.09.2020: Kante, Jorginho, Mata, King, Dias, Garcia

Image
CHANZO CHA PICHA, REX FEATURES Manchester United imewasiliana na washauri wa kiungo mkabaji wa Ufaransa N'Golo Kante kuhusu hatua ya kuondoka Chelsea, lakini makubaliano yoyote na mchezaji huyo, 29, huenda yakapelekea kupunguzwa pakubwa kwa mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki. (Mirror) Lazio huenda ikataka kuwasajili viungo wawili wa Manchester United, Juan Mata, 32, na Mbrazili Andreas Pereira, 24. (Sun) Leicester City wanapanga kumsajili beki wa kati wa Torino, 23, Mbrazili Gleison Bremer, ambaye pia anawindwa na klabu ya Everton. (Football Insider) CHANZO CHA PICHA, REUTERS Maelezo ya picha, Joshua King Mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Joshua King, 28 anawindwa na Tottenham Hotspur wakati huu ambapo klabu hiyo inataka kumsajili mshambuliaji kabla ya siku ya ukomo ya uhamisho. (Telegraph - subscription required) Spurs pia wanapiga hesabu za kumsajili Kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya ya Uswizi Haris Seferovic, 28. (Football Insider) Tetesi za sok...

BAADHI YA SHERIA ZA MPIRA WA CHANDIMU).

Image
BAADHI YA SHERIA ZA MPIRA WA CHANDIMU). . 1.Mchezaji mnene zaidi atakuwa Golikipa. 2.Mechi haitaanza mpaka mwenye Mpira awe amemaliza kazi za nyumbani kwao, ikitokea wachezaji wengine wanautaka Mpira huo basi sharti wamsaidie kufanya kazi zake ili ziishe mapema na mechi kuanza. 3.Viatu hutumika kuonyesha alama ya goli linapoanzia na linapoishia. 4.Ikitokea penati mchezaji ambae si Golikipa ataruhusiwa kukaa golini kisha ataendelea kucheza nafasi yake ya mwanzoni baada ya penati kupigwa. 4.Hakuna refarii, na ikitokea mchezaji kashika basi wale wababe wataamua kama ni penati au si penati. 5.Mchezaji ataweza kuingia tena kwa mara ya pili bila ya kujali kama tayari alishafanyiwa mabadiliko (substitution). 6.Ikitokea Mpira umepigwa umbali mrefu au umeingia kwenye fensi ya mtu basi wachezaji wote watapaswa kwenda kuusaka na yoyote atakayeonekana kutegea hataruhusiwa tena kucheza baada ya Mpira kupatikana. 6.Wale watakaoanza kufungwa goli watalazimika kuvua mashati yao ili kutoa tofauti baina...

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 27.09.2020: Aouar, Rice, Rudiger, Fati, Torreira, Kante

Image
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Houssem Aouar Lyon itataka euro milioni 50 sawa na pauni milioni 46 kwa makubaliano yoyote yanayomhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Houssem Aouar, 22, baada ya kukataa ofa ya Arsenal ya euro milioni 36. (RMC Sport) Arsenal iko tayari kuongeza ofa yao kwa Lyon wakimlenga Aouar hadi pauni milioni 36.5, na uwezekano wa nyongeza ya ziada ya pauni milioni 9. (Football London) Chelsea itatoa ofa rasmi ya zaidi ya pauni milioni 40 kwa Declan Rice na inaamini kwamba hiyo itatosha kumsajili kiungo wa kati wa England, 21 - kwasababu West Ham inahitaji pesa. (Sun on Sunday) Lakini Hammers inamatumaini ya kumsajili mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 27, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Sun on Sunday) CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Ansu Fati akiwa amelala uwanjani Barcelona imekataa ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Uhispania, 17, Ansu Fati ya euro milioni 125, pamoja na nyongeza ya euro milioni 25. (Marca - in Spanish) Manchester Unite...