Tetesi za soka Ulaya Jumapili 27.09.2020: Aouar, Rice, Rudiger, Fati, Torreira, Kante


Houssem Aouar
Maelezo ya picha,

Houssem Aouar

Lyon itataka euro milioni 50 sawa na pauni milioni 46 kwa makubaliano yoyote yanayomhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Houssem Aouar, 22, baada ya kukataa ofa ya Arsenal ya euro milioni 36. (RMC Sport)

Arsenal iko tayari kuongeza ofa yao kwa Lyon wakimlenga Aouar hadi pauni milioni 36.5, na uwezekano wa nyongeza ya ziada ya pauni milioni 9. (Football London)

Chelsea itatoa ofa rasmi ya zaidi ya pauni milioni 40 kwa Declan Rice na inaamini kwamba hiyo itatosha kumsajili kiungo wa kati wa England, 21 - kwasababu West Ham inahitaji pesa. (Sun on Sunday)

Lakini Hammers inamatumaini ya kumsajili mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 27, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Sun on Sunday)

Ansu-Fati-lying-on-pitch.
Maelezo ya picha,

Ansu Fati akiwa amelala uwanjani

Barcelona imekataa ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Uhispania, 17, Ansu Fati ya euro milioni 125, pamoja na nyongeza ya euro milioni 25. (Marca - in Spanish)

Manchester United bado inamfukuzia beki wa kushoto wa Porto raia wa Brazilian Alex Telles - na inasemekana kwamba inamatumaini makubwa kwamba makubaliano juu ya mchezaji huyo, 26, yatafikiwa hivi 

United pia imejiunga na wengine wanaopania kumpata mchezaji wa Argentina, 16, Alex Luna, anayechezea Atletico Rafaela nyumbani kwao, na iko tayari kukabiliana na AC Milan kuhakikisha inamsajili - hata ingawa huenda asipatikane hadi 2022.(Sunday Mirror)

Arsenal's Lucas Torreira was injured in the FA Cup tie at Portsmouth
Maelezo ya picha,

Lucas Torreira mchezaji wa Arsenal

Torino haina haja tena ya kumsajili mchezaji wa Arsenal Lucas Torreira na ingawa Atletico Madrid bado inaonesha nia ya kutaka kumsajili, Gunners ingependelea kufikia makubaliano ya kudumu kwa kiungo huyo wa kati wa Uruguay, 24. (Football London)

Inter Milan imejitayarisha kutoa mlinzi wake wa Slovakia Milan Skriniar, 25, na kiungo wa kati wa Croatia Marcelo Brozovic, 27, kwa Chelsea ikiwa na matumaini ya kumsajili kiungo wake wa kati N'Golo Kante. (90 min)

Leeds United imejitayarisha kutoa ofa yao kwa Norwich City ikilenga aliyekuwa mchezaji wa Under-21 wa England, winga Todd Cantwell, 22. (Football Insider)

Chelsea midfielder N'Golo Kante
Maelezo ya picha,

N'Golo Kante kiungo wa kati wa Chelsea

Lakini mkurugenzi wa Inter amepuuzilia mbali makisio kwamba wanataka kumsajili Kante ambaye awali alicheza chini ya kocha Antonio Conte akiwa Stamford Bridge. (Express)

Mshambuliaji wa Liverpool, 20, Rhian Brewster anataka kuzungumza na Crystal Palace kuhusu uwezekano wa uhamisho kwa kima cha pauni milioni 20 ijapokuwa Sheffield United na Aston Villa pia nao wanamkodolea macho mchezaji huyo wa England wa kimataifa wa Under-21. (Sun on Sunday)

Baada ya kuwa kwenye majadiliano na Liverpool juu ya Brewster na Arsenal kwasababu ya mshambuliaji Folarin Balogun, 19, Sheffield United sasa hivi inafuatilia kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Uingereza Daniel Sturridge, 31, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Trabzonspor mnamo mwezi Machi. (Mail)

Harry Wilson and Rodrigo De Paul
Maelezo ya picha,

Harry Wilson na Rodrigo De Paul

Udinese imeiarifu Leeds United kuwa itakubali tu ofa ya pauni milioni 40 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Argentina Rodrigo de Paul, 26. (90 min)

Manchester City imejitayarisha kutoa makubaliano mapya kwa kiungo wa kati wa England Phil Foden, na kuongeza mshahara wa mchezaji huyo wa miaka 20 kutoka pauni 30,000 kwa wiki hadi zaidi ya pauni 150,000. (90 min)

Liverpool itafanya mazungumzo na mlinzi Motherwell Sam Campbell baada ya ofa ya Leeds United na Brighton kukubaliwa kwa ajili ya mchezaji huyo, 16. (Football Insider)

Luka Jovic
Maelezo ya picha,

Luka Jovic akichezea Eintracht Frankfurt katika ligi ya Europa

Real Madrid inataka kumtoa Luka Jovic kwa mkopo lakini klabu chake cha awali Eintracht Frankfurt hakiko tayari kufikia makubaliano hayo kwa mshambuliaji huyo wa Serbia, 22. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Rennes, Eduardo Camavinga, ambaye alijitokeza kwa mara ya kwanza Ufaransa mwezi huu akiwa na umri wa miaka, 17, yuko tayari kusubiri hadi Julai 2021 kujiunga na Real Madrid, huku mabingwa hao wa Uhispania wakiwa wameshafanya mazungumzo. (Marca - in Spanish)

Hertha Berlin imemkodolea macho mshambuliaji wa Ujerumani Mario Gotze, 28, baada ya kukamilisha mkataba wake na Borussia Dortmund mwisho wa msimu uliopita season. (Bild - in German)

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.09.2020: Kante, Jorginho, Mata, King, Dias, Garcia

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.09.2020: Sancho, Jovic, Alaba, Tagliafico, Lamptey

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.10.2020 Alli, Aouar, Rudiger, Torreira, Gray