Posts

Showing posts from October, 2019

USHAWAHI KUFANYIWA HIVI

Image
Nakumbuka wakati Ex wangu aliponikataa na kukatisha mahusiano na mimi bila kumtendea kosa lolote, nilichanganyikiwa sana. Niliumia moyo. Nilihisi kusalitiwa mno pale alipoanza kutembea na mtu mwingine punde tu baada ya kuniacha. Nilijihisi sina thamani tena, niliyachukia mapenzi na nikajichukia na mimi mwenyewe. Niliapa kutopenda tena, niliumwa mno, nilikua sili chakula, vidonda vya tumbo vikachachamaa, nilipoteza uzito. Nilijiona sifiti tena kwa marafiki zangu waliokuwa na wapenzi wao, walipokua wakinialika katika mitoko yao wakiwa na wapenzi wao, mimi sikwenda! Nijiona sio mwenzao. Na nilijiuliza maswali mengi sana kama, kwanini naumizwa mimi kila siku? Kwanini amesahau mazuri yote niliyomfanyia na nyakati zote tulizofurahi pamoja? Kwanini nisijifunze kupotezea kama mahusiano yalopita? Nilijiuliza maswal mengi lakini wala sikuwa na majibu ya kujiridhisha, sana sana nilizidi kukonda sana na mawazo! Ila siku moja asubuhi nilipoamka kutoka ktk usingizi wa kuunga unga baada y...

MWANAUME WA KWELI NDIO HUYU

Image
Mwanaume mjanja huwa hakopi pesa Benki  ya kufungia harusi hata siku moja bali hutengeneza wazo bora la kumuingizia pesa kwa ajili ya maisha yake bora ya baadaye ndipo hutengeneza  wazo la kufunga ndoa bora na sio harusi nzuri. Mwanaume mjanja huwa hakopi pesa Benki kwa ajili ya kununulia gari, bali hutumia mfumo wa Kondakta wa Daladala kukusanya kila pesa ndogo anayopata kisha pesa ndogo ambayo imewekwa kwa malengo na muda mrefu  huzalisha na kuwa pesa kubwa ambayo huwekaza na kuzalisha pesa ya kununua gari bila mkopo. Mwanaume mjanja huwa hamuhongi pesa mwanamke hata siku moja bali, humjenga mwanamke kifikra na mwanamke kubadili mtazamo wake kutoka kuomba pesa mpaka kuwa mwanamke muwajibikaji na nguzo thabiti ya mahusiano bila kuomba pesa. Mwanaume mjanja huwa sio mnafiki wala muongo hata siku moja, mwanaume mjanja huwa ni mwenye kauli thabiti na anayesimamia ukweli na uwazi na mwenye mawazo ya haki na usawa kwa kila jambo. Mwanaume mjanja akiongea na mtu huw...

UGONJWA WA PID

Image
#PID ni hali ya kututumka au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke, sehemu hizi ni kama mirija ya uzazi au ovary ambako kunasababishwa na magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono. Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix). Maambikizi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata Ectopic pregnancy ambayo ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija. Kama bado hauja update app hii, basi Fanya sasa tumeongeza mambo mapya ndani ya app hii hakikisha unaenda Playstore kisha unaupdate

SIFA ZA MWANAMKE ANAYEPENDA SANA PESA

Image
Hongereni wanawake tunawapenda Sana kwani ninyi ndio furaha yetu, amani yetu, utulivu wetu. Bila ninyi dunia hatujui ingekuwaje. Basi baada ya machache hayo nirejee kunako mada. Siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la mamilioni ya wanawake wanaopenda Sana pesa kuliko kitu chochote. Jambo hili lilianza Kama mzaha lakini kwa sasa hakuna wakuuzima moto huu. Kupenda pesa sio vibaya ila kuipenda sana kiasi kwamba mtu yupo radhi auze utu wake na kuudharau kabisa uanamke wake. Kama hiyo haitoshi wanawake wengi wanaopenda pesa ndio huwa chanzo cha maangamizi katika familia. Zifuatazo ni sifa bainifu za wanawake wanaopenda Sana pesa;- 1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao. Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine k...