Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.10.2020 Alli, Aouar, Rudiger, Torreira, Gray
Tottenham wamekataa ofa ya mkopo wa pauni milioni 1.5 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya mlinda mlango Dele Alli na mchezaji huyo, 24, anajiandaa kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya London. (Guardian)
Lakini klabu ya Ligue 1 watakuwa wanaandaa ofa ya mwisho ya mkopo kwa ajili ya Alli. (Telegraph)
Antonio Rudiger alisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Mabara mwaka 2017 nchini Urusi
Spurs pia imeweka ofa ya mkopo kwa ajili ya mlinzi Antonio Rudiger, 27, anayekipiga Chelsea, wakati mazungumzo yakiendelea kati ya mahasimu hao wa London. (Nicolo Schira via Express)
Lucas Torreira wa Arsenal huenda akaondoka klabu hiyo
Arsenal wamekubali dili la mkopo kwa ajili ya mlinzi wa Uruguay Lucas Torreira, 24, kwenda Atletico Madrid, na hatua hiyo itawaruhusu kumsajili kiungo wa kati Hossem Aouar, 22, kutoka Lyon. (AS,via Mirror)
Houssem Aouar
Paris Saint-Germain wanaweza kudhoofisha mpango wa washika bunduki kumshawishi Aouar baada ya pia kuingia kwenye mazungumzo ya kumnasa Mfaransa huyo. (L'Equipe,via Metro)
Leicester City inajiandaa kutoa ofa ya mkataba mpya kwa winga Harvey Barnes, 22. (Telegraph)
Alonso ni beki wa kushoto wa Chelsea
Inter Milan wanajiandaa kumnasa beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso, 29. (Sky Sports)
Leicester City wako tayari kupokea ofa kwa ajili ya winga Demarai Gray, ambaye yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo. (Mirror)
Demarai Gray (kushoto)
Manchester United wanajaribu kumsajili winga wa Atalanta na Ivory Coast Amad Traore, 18. (Manchester Evening News)
Fulham wanajaribu kuwanasa mabeki wa kati wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili tarehe 5 mwezi Oktoba, huku klabu ikimfuatilia mlinzi wa PSV Eindhoven Timo Baumgartl, 24. (Telegraph)






Comments
Post a Comment