UKIFANYA HAYA BASI MAFANIKIO NI YAKO KABISA!!!
akikwambia hivi na wewe mwambie mbona na wewe rika ni moja kabisa na Bakhresa 😀😀😀😀
Hello karibu tena, hayo maneno ya juu,tunashtuana tu kidogo ila usimjibu hivyo mzazi wako, kumbuka anachokifanya yeye ni chema sana.
Leo hebu tuangalie kidogo, nikifanya nini?? Itanisaidia kupiga hatua moja kwenda nyingine.
Nikwambie kitu kimoja ndugu yangu, kwenye mafanikio, tunaanza kuyapima vizuri kwenye akili yako kwamba unawaza nini, je unawaza hasi tu au ni mtu wa kuwaza chanya!!!
Mambo yafuatayo yatakusaidia sana ili kufikia MAFANIKIO.
1.JIAMINI.
Ooh hili ni jambo la msingi sana, ukikosa kujiamini hatutojua msimamo wako, na tusipojua msimamo wako ni rahisi sana kukuangusha.Hivi si ushawahi kuona vijana wa mtaani, japokuwa wanasema wao ni wajanja ila kuna mdada wanashindwa kabisa(Kumtongoza) hii yote ni faida ya msimamo thabiti kwa mwenye kujiamini.
Ukiwa na wazo ambalo unalisimia na unadhani litakutoa kimaisha basi jiamini, simamia malengo yako.
2.KUWA MTU WA MAOMBI
Amini usiamini ,imani ni msingi wa kila kitu.Hao unaowaona wamefanikiwa kuna wanachokiamini na kukiabudu,usiwe mnyonge sana anza kufanya Ibada huku ukimwomba Mungu akusaidie katika harakati unazozifanya kila siku, kumbuka usijiweke wa kawaida sana, Lazima utakuwa unatumikia mmoja wa mabwana Hawa Mungu au shetani. Inakupasa kusimama sana kwenye imani kuna watu wengine wanaweza tamani kukuangusha Kwa kutumia nguvu za kishetani ni bora kuwa na imani thabiti.
3.UWE MBUNIFU.
Hapa patamu kweli, ubunifu ubunifu ubunifu, acha tu niutaje tena ubunifu, Ngoja nikwambie ubunifu Una radha yake bwana, yaani ukitaka kuona mambo matamu Fanya katika hali ya ubunifu.
Unajua ubunifu unaweza kuufanya na hata ukakupunguzia gharama katika shughuli yako.
Siku hizi mambo madogo yanakupa jina kubwa lakini ufanye katika ubunifu.
Hata kama unafanya vitu ambavyo vipo lakini usifanye kama wengine wanavyofanya hapo utakuwa umeondoa maana ya ubunifu.
Kwa Mfano mtu anaweza kuweka kwamba Mda huu wateja wangu nawapunguzia sh 150 katika kilo ya mchele, hapo utatengeneza jina kubwa sana kwa watu.Alafu mda ukipita bei inaendelea kama ya awali.
Kikubwa katika ubunifu ni kwamba unapata jina kirahisi sana, si unajua ukiwa na jina na biashara yako imeshapata soko.
4.UWE MWENYE FURAHA
Ndugu usijiweke wa majonzi sana, jaribu kujitengenezea furaha katika maisha yako, hii itakusaidia sana katika njia ya mafanikio yako.
5.JIFUNZE KWENYE MAKOSA
Umekaa Mda wote unasoma mafanikio ya wengine tu, sawa ni jambo jema sema kuna wengine wanapata motisha tu lakini wanashindwa la kufanya.
Tunasema njia nzuri ya kujifunza ni kwenye makosa, aidha makosa yako au hata ya wengine hakika kwa njia hiyo utaweza kufanikiwa, angalia unapokosea ili usimame upya.
6.USIKATE TAMAA/USICHOKE KUJARIBU
Kujaribujaribu kunachoshaaaaa, mmh ni kweli kunachoshaaaaa lakini, hebu tuone endelea kuchoka kujaribu ili uzidi Kuwa mtumwa lakini kama unataka uwe na ngome yako yaani utawala wako, usichoke kujaribu.
Jipe moyo mwenyewe kwamba siku moja utaweza, siku moja mambo yatajipa haina haja kukata tamaa.
Simama ndugu yangu, safari ni kama imeanza, dereva mzuri ndiye atakayeimaliza, najua umeamua Kuwa dereva mzuri, unakata tamaa Kwa nini, au maneno yao ya kukudhofisha yanakukondesha, achana nao utawaajiri baadae, kuwa mpole pambana hakika unaweza.
7.UKIAMUA FANYA KWELI.
Ndio najua nifanye nini nifanikiwe, ndio nimeshajua nitafanya mradi gani au nitaanzia wapi, kweli nimeshajua.
Watu wamekufa na mawazo yao, haina faida wala maana yoyote kama unajua lakini unashindwa kuchukua hatua hata kidogo.
Hicho Hicho ulichonacho Hebu anza nacho.
Nikuibie siri hakuna mtu anapenda kuwa sehemu ya maisha yako wakati wa shida,wote wanapenda kuwa nawe wakati wa raha.Kwa maana hiyo nakwambia waharibifu ni wengi sana wamekuzunguka yawezekana hata huyo unayecheka naye, ni kama anakupenda vile kumbe hapendi kukuona unafanya kweli.
Nisikuchoshe ukiamua amua kweli #ANZA HAPO ULIPO.
***Hakuna siku utapata kila kitu kuanzisha wazo lako, usijidanganye anza ulipoo, watakusaidia wakiona kuna mwanga katika hilo ulilolianza***
utakuwa mchoyo sana Kama unashindwa kumwambia mwenzako adownload app hii inayoitwa MCHONGO MPYA


Comments
Post a Comment