WALINZI WA ROSTAM NI KWELE

Baada ya kukaa kimya kwa muda bila kuachia wimbo mpya hatimaye kundi la Rostam leo limedondosha ngoma yao mpya waliyoshirikiana na mkali Ney wa Mitego, ngoma hiyo mpya ambayo wameitambulisha kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM wameitambulisha kwa style ya kitofauti na vile ilivyozoeleka.
Loading…Roma na Stamina waliambata na watu ambao wamevalia mavazi ya kiganga ya kienyeji huku watu hao wakiwa wamebebelea vitendea kazi vya kiganga ambao Rostam wamewaita watu hao kuwa ni walinzi wao na kuwafananisha na kama Bodyguard wanaotumiwa na wasanii wengine wakati wakienda kutambulisha ngoma zao.
…>>>“Hawa unaowaona ni walinzi wetu sio waganga na tumekuja na hawa kutokana na kile ambacho tumewaletea leo, mara nyingi wasanii wakija hapa kwenye XXL huwa wanakuja na watu waliovaa nguo nyeusi na wamenuna ila sisi tumeamua kuja na walinzi wetu wa kitofauti, kumbuka Rostam sisi tumetokea Tanga na Morogoro hivyo hawa ni mizimu yetu” Rostam

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.09.2020: Kante, Jorginho, Mata, King, Dias, Garcia

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 30.09.2020: Sancho, Jovic, Alaba, Tagliafico, Lamptey

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 02.10.2020 Alli, Aouar, Rudiger, Torreira, Gray