USHAWAHI KUFANYIWA HIVI
Nakumbuka wakati Ex wangu aliponikataa na kukatisha mahusiano na mimi bila kumtendea kosa lolote, nilichanganyikiwa sana. Niliumia moyo. Nilihisi kusalitiwa mno pale alipoanza kutembea na mtu mwingine punde tu baada ya kuniacha.
Nilijihisi sina thamani tena, niliyachukia mapenzi na nikajichukia na mimi mwenyewe. Niliapa kutopenda tena, niliumwa mno, nilikua sili chakula, vidonda vya tumbo vikachachamaa, nilipoteza uzito.
Nilijiona sifiti tena kwa marafiki zangu waliokuwa na wapenzi wao, walipokua wakinialika katika mitoko yao wakiwa na wapenzi wao, mimi sikwenda! Nijiona sio mwenzao.
Na nilijiuliza maswali mengi sana kama, kwanini naumizwa mimi kila siku? Kwanini amesahau mazuri yote niliyomfanyia na nyakati zote tulizofurahi pamoja? Kwanini nisijifunze kupotezea kama mahusiano yalopita? Nilijiuliza maswal mengi lakini wala sikuwa na majibu ya kujiridhisha, sana sana nilizidi kukonda sana na mawazo!
Ila siku moja asubuhi nilipoamka kutoka ktk usingizi wa kuunga unga baada ya kuwa na usiku mrefu wa mawazo na majonzi, nilijiuliza maswali haya; kwanini najiumiza moyo wangu, kwanini ninalia? Kwanini sili chakula? Nikaja kugundua kuwa hakuna jambo kubwa la kuhofia na kunitia simanzi.
Alikuwa ni mgeni tu maishani mwangu nimekutana nae ukubwani ambae akanifanya nimpe mapenzi yangu yote na hisia zangu zote na akaondoka na kuniacha. Sijapoteza Baba wala mama, wala wadogo zangu na kaka Zangu ni yeye tu! Naumia kwa jambo ambalo halipo tena!
Ingeonekana kama ni hasara kwangu kumpoteza yeye ila kiukweli hasara ni kwake! Amempoteza mtu ambae alimpenda kwa dhati, kwamba sidhani kama atatokea mtu atakae kuja kumpenda kama mimi nilivyompenda! Amenipoteza mimi ninayejua maana halisi ya maisha na mwenye njaa ya mafanikio!
Kuanzia hapo nikagundua kuwa kutumia muda wangu mwingi kumuwaza yeye, kujikumbushia zile nyakati njema pamoja nae, mipango kabambe ya baadae tuliyopanga pamoja na mengineyo ni upotezaji wa muda wangu wa thamani tu
Nikaacha kulia na kufuta kumbukumbu zote na nikarudi katika hali yangu ya kawaida. Nikaanza kutumia muda wangu mwingi katika kutafuta pesa, kusoma vitabu, kumtumikia Mungu wangu, kuwa karibu na familia yangu, kuwaza kuhusu ndoto zangu za biashala na mambo mengine ambayo yatanisaidia
Hapo ndipo kupona kwangu na maumivu ya mapenzi kulianza. Nikagundua kwamba alikuwa ni ukurasa tu katika kitabu changu cha maisha. Kwamba nilihitaji ujasiri wa kuufunga huo ukurasa na kufungua mwingine.
Haikuwa rahisi kwangu, ilinichukua muda mrefu sana ila niliweza. Mwanzoni kila nilipokuwa nikicheki DP yake watsapp, pcha zake fb akiwa na mtu wake mpya nilikuwa nikiumia sana. Ila baadae nikaona ni jambo la kawaida na wala haikuniumiza tena. Neema ya Mungu ilinishukia, nikatambua thamani yangu tena.
Ndio, ni vigumu sana kumsahau yule uliempenda pale anapokuacha, ila ukiamua kusonga mbele inawezekana. Kamwe usifikiri hautakuja kupona na maumivu ya kuachwa au kusalitiwa. Utafanikiwa tu! Ni jambo la muda, ujasiri na kutambua thamani yako tu.
Usifikiri kwamba hutapenda tena, utapenda tu wakati wako utakapofika na utakuwa mtu mwenye furaha tele kama mimi, ni kama ilivyo Kila jambo na wakati wake na majira yake.......🍒
Tunakukumbusha nenda Playstore andika Mchongo Mpya kisha update app hii, tumeongeza mambo mengiiiiii mapya ya muhimu.

Comments
Post a Comment