MWANAUME WA KWELI NDIO HUYU
Mwanaume mjanja huwa hakopi pesa Benki ya kufungia harusi hata siku moja bali hutengeneza wazo bora la kumuingizia pesa kwa ajili ya maisha yake bora ya baadaye ndipo hutengeneza wazo la kufunga ndoa bora na sio harusi nzuri.
Mwanaume mjanja huwa hakopi pesa Benki kwa ajili ya kununulia gari, bali hutumia mfumo wa Kondakta wa Daladala kukusanya kila pesa ndogo anayopata kisha pesa ndogo ambayo imewekwa kwa malengo na muda mrefu huzalisha na kuwa pesa kubwa ambayo huwekaza na kuzalisha pesa ya kununua gari bila mkopo.
Mwanaume mjanja huwa hamuhongi pesa mwanamke hata siku moja bali, humjenga mwanamke kifikra na mwanamke kubadili mtazamo wake kutoka kuomba pesa mpaka kuwa mwanamke muwajibikaji na nguzo thabiti ya mahusiano bila kuomba pesa.
Mwanaume mjanja huwa sio mnafiki wala muongo hata siku moja, mwanaume mjanja huwa ni mwenye kauli thabiti na anayesimamia ukweli na uwazi na mwenye mawazo ya haki na usawa kwa kila jambo.
Mwanaume mjanja akiongea na mtu huwa anazima simu awapo kwenye mazungumzo ili asikilize zaidi kuliko kuongea.
Mwanaume mjanja huwa anatumia elimu yake kwa manufaa ya jamii na sio ubinafsi wake, mwanaume mjanja huwakumbuka wazazi wake kwa Swala na Dua na daima huwatembelea wazazi wake mara kwa mara.
Mwanaume mjanja hu save pesa kuanzia january mpaka December na hutenga likizo ya kupumzisha nafsi, mwili na ubongo na kutizma fursa za biashara akiwa likizo, Mwanaume mjanja huwa hafanyi anasa na starehe sababu yeye amezitawala anasa, starehe, pombe na wanawake.
Mwanaume mjanja hutambua kufanya kazi kwa bidii na weredi ni chanzo cha mafanikio na pia hutambua furaha ni chanzo cha afya bora na njema.
Usiwachukie watu ambao wanakuonea wivu, lakini waheshimu watu wanao kuonea wivu kwa sababu ndio ambao wanafikiri wewe ni bora zaidi yao.
Hard work and prayers lead to success
#YouTube @SalvaOnlineTV

Comments
Post a Comment