Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.09.2020: Kante, Jorginho, Mata, King, Dias, Garcia
CHANZO CHA PICHA, REX FEATURES Manchester United imewasiliana na washauri wa kiungo mkabaji wa Ufaransa N'Golo Kante kuhusu hatua ya kuondoka Chelsea, lakini makubaliano yoyote na mchezaji huyo, 29, huenda yakapelekea kupunguzwa pakubwa kwa mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki. (Mirror) Lazio huenda ikataka kuwasajili viungo wawili wa Manchester United, Juan Mata, 32, na Mbrazili Andreas Pereira, 24. (Sun) Leicester City wanapanga kumsajili beki wa kati wa Torino, 23, Mbrazili Gleison Bremer, ambaye pia anawindwa na klabu ya Everton. (Football Insider) CHANZO CHA PICHA, REUTERS Maelezo ya picha, Joshua King Mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Joshua King, 28 anawindwa na Tottenham Hotspur wakati huu ambapo klabu hiyo inataka kumsajili mshambuliaji kabla ya siku ya ukomo ya uhamisho. (Telegraph - subscription required) Spurs pia wanapiga hesabu za kumsajili Kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Benfica na timu ya ya Uswizi Haris Seferovic, 28. (Football Insider) Tetesi za sok...
Comments
Post a Comment